Palikuwapo na njama ya Benki kadhaa kwenye soko la ubadilishanaji wa fedha inayolenga kuendelea kuishusha thamani ya shilingi ya Kenya-Patrick Njoroge

Gavana wa Benki kuu nchini Patrick Njoroge,amefichua kwamba palikuwapo na njama ya Benki kadhaa kwenye soko la ubadilishanaji wa fedha inayolenga kuendelea kuishusha thamani ya shilingi ya Kenya na hivyo kuitumbukiza katika mgogoro mkubwa wa kiuchumi sawa na ule wa sakata ya Golden Bag.

Njoroge ambaye alisita kuweka wazi majina ya wanaohusika na Benki hizo,amesema kwamba njama hio ndio iliosababisha kushuka kwa thamani ya shilingi ya kenya dhidi ya dola katika soko la kimataifa.

Amesema kwamba mpango wa watu hao ulilenga kuilaghai mabilioni ya fedha serikali,na hivyo kuiacha katika hali mbaya ya kiuchumi sawa tu na jinsi mabilioni hayo yalivyoibwa wakati wa sakata ya Golden Bag ambapo fedha hizo zilihusishwa na biashara ya dhahabu na almasi.

Akizungumza mbele ya wabunge wakati wa kongamano jijini Nairobi kuhusu sababu za shilingi ya kenya kuendelea kudidimia katika soko la kimataifa,Njoroge amesema kwamba watu hao wanaoshirkiana na mtandao wa uhalifu wa kifedha waliolenga kufanikisha hilo,licha ya dola yenyewe kuimarika kote duniani. Njoroge ambaye alimiminiwa sifa kutokana na jinsi alivyofanikisha matumizi ya noti mpya bila ya uchumi kuyumba yumba,aidha amewahakikishia wabunge kwamba kenya ina dola za kutosha kubadilisha pesa za kenya,akifichua kwamba Benki kuu ilifanikiwa kuigundua njama hio miezi miwili iliopita na kuikabili.

Leave a Reply