You are currently viewing Rais William Ruto kulihutubia kongamano la 77 la UN jijini New York Marekani.
Rais William Ruto

Rais William Ruto kulihutubia kongamano la 77 la UN jijini New York Marekani.

Rais William Ruto leo hii anatarajiwa kulihutubia kongamano la 77 la kimataifa UN linaloendelea jijini Newyork uko marekani.

Rais Ruto anatarajiwa kuzungumzia kuhusu mabadiliko ya hali ya anga na athari zake vilevile ukame unaoendelea kushuhudiwa katika upembe wa afrika ikiwamo kenya.

Wakti uo huo Rais Ruto atakaehutubu kwa mara ya kwanza kabisa katika kongamano hilo akiwa rais,anatarajiwa kukutana na viongozi wengine wa kimataifa ambapo watajadili kuhusu uhusiano wa kenya na mataifa mbalimbali .

Ruto vilevile atakutana na marais wengine kutoka afrika ambapo maswala mengine muhimu yatajadiliwa.

Katika hotuba ya ufunguzi wa kongamano hilo,katibu mkuu wa umoja wa mataifa UN Antonio Guteresh,ameitaja mabadiliko ya anga kama janga kuu linaloikumba dunia kwa sasa. Guteresh kadhalika amesema kwamba matatizo mengine ni kama vile hali ngumu ya uchumi ulimwenguni.

Leave a Reply