Kinara wa ODM Raila Odinga leo ijumaa anatarajiwa kuendeleza misururu ya mikutano yake ya azimio la umoja katika kaunti ya uasin gishu na kaunti nyingine za kaskazini mwa bonde la ufa.
Baada ya kutua rasmi hapo jana mjini Eldoret ,Raila alikaribishwa na mratibu mkuu wa shughuli zake za kisiasa za eneo hili ambaye pia ni gavana wa Elgeyo Marakwet Alex Tolgos .
Viongozi wengine waliomkaribisha ni Pamoja na mwanachama wa baraza la ODM na mwandani wa Raila wa mda mrefu Kipkorir Menjo na mwenyekiti wa ODM tawi la Uasin Gishu David Songok.
Miongoni mwa mipango ilioratibiwa ni kufunguliwa upya kwa ofisi za ODM ,mkutano na wakulima na ujumbe kutoka kaunti za eneo hilo.
Jana alhamisi raila alikua katika kaunti ya turkna ambapo alirejelea ahadi zake za kuwainua wakenya maskini kupitia ruzuku ya shilingi alfu sita ,kadhalika kuwahaidi wakaazi wa Turkana maendeleo makubwa zikiwemo haki za kimsingi,chakula na afya.